3, ఆగస్టు 2016, బుధవారం

Kabla hujanunua power bank zingatia haya



Tatizo la umeme bado linasumbua maeneo mengi Tanzania kwa hiyo watu wengi wamekua wakiangalia
njia mbadala kuhakikisha simu, laptop au vifaa vingine vikiwa na chaji.

Lakini kwa sasa kuna Power banks ambazo zinasaidia kuchaji wakati ambapo kuna tatizo la kukosa umeme au chanzo cha kuchajishia, hata hivyo kabla ya kununua power bank ni muhimu kuyajua haya.

Uzito
Power banks zinakuja katika uzito na ukubwa tofauti. Unashauriwa kununua yenye uzito unaobebeka ili isiwe mzigo sana pale unapokua umeibeba.

Brand (Jina)
Jina la power bank unayotaka kununua ni muhimu sana. Tayari iko wazi kua majina makubwa ndiyo ya uhakika kwa ubora, kudumu na kuendana na thamani ya pesa yako. Baadhi ya kampuni zinaweza kua ghali lakini ndio zenye uhakika wa kudumu. Pamoja na haya yote unatakiwa kuangalia jina la kampuni haliko taofauti na kasha (package) ili usijikute unauziwa feki.

Power Capacity (Nguvu)
Kwa kila power bank unayotaka kununua inatakiwa iwe mara 2.5 zaidi ya nguvu ya simu yako. Kwa maneno mengine kama betri ya simu yako ni 4000mAh, unatakiwa ununue power bank ya 10000mAh. Utatumia 6000mAh pekee kuchajia kitu ambacho ni bora kuliko kutumia yenye uwezo sawa na simu yako.

Ubora
Nchi nyingi za kiafrika hususani Tanzania zimekua ni jalala la bidhaa zisizo na viwango ikiwemo power banks. Pamoja na kuzingatia brand pia ni muhimu kua makini usije kununua feki kwa sababu ni nyingi sokoni.

*Hata hivyo kuna taarifa kua Power Banks zinapunguza uwezo wa betri ya simu yako, ni muhimu kukaa unafahamu hili!!

0 కామెంట్‌లు:

కామెంట్‌ను పోస్ట్ చేయండి